Kenya's No 1 GhettoRadio

Baba Dogo wasee wamebonda juu Grao imenyakuliwa

0

Wasee mtiech ya Baba Dogo yenye iko Ruaraka constituency wanazusha after wakanjwe eviction notice.

Hio notice ilikanjwa na Kenafric industries wenye ndio owners wa ng’ondo penye grao ya Baba iko. 

Hio gazette notice ni ya February 22, 2022, na wasee wamechapiwa kusaree activities asapo, wabomoe buildings ziko hapo na ku vacate within miezi utat kuanzia date of notice.

Wasee wa baba wamebonda wakidai hio grao ni ya community, penye ndimu huguzwa hadi sport activities zingine, hadi mapoliticians huitumia kwa campaigns.

Wanadai ime help kuzuia mayut wasiingile crime juu wana nurture talents zao hapo, hadi kuna ma bukla za tispo huguzia asapo.

Hizo teams huchezea FKF league, MYSA League, Zebstrong Kids league, alafu Tourna ya Michael Olunga. 

Former MCA wa mtaa, Shadrack Juma, anadai kesi ya hio shake ilifikishwa Nairobi County Assembly akiwa offe na directive ikadai ni public utility.

Majuzi tu vibandaski zilikua kwa hio grao zilibomolewa.

By Nicanory Muhando

Comments
Loading...