Kenya's No 1 GhettoRadio

Dingo aliponea mob justice kudoze zangaro 6 years

0

Kuna dingo mwenye ni 19 years mwenye aliruka hadi ndani ya dangulo mtaani L.A kuhepa team building ya mob wenye walikuwa manyu yake after waliwanyuria maarif wake mbexe, ata serve nditni miaka sita for attempted robbery.

James Okello ali sentesiwa zangaro na judgiko Abdul Lorot wa mbwenya Kibera after alikubali charges.

Akiwa kwa mbogi ya maarif wake mbexe, walitry kumnyafura Rose Nduku Kioko tenje yake Kitengela road yenye iko Langata on October 11th.

Magithaa ilikuwa ma aftee na hio mbogi walikuwa kwa nduthi.

Walimstab kwa thayo na tumbo, akapiga nduru na chogi alikuwa karibu akamuok.

Huyo chogi alimkeiyo mjamo na rungu, mraia wakamokre scene na ndio mob justice ikaanza.

Okello aling’ada hadi kwa keja iko karibu, ni mambaru walimsave otherwise mob walikuwa wanatry kuvunja ndani wamnyurie.

Okello akijitetea alidai landlord alimchuja kejani juu ya rent sasa walikuwa wanasakanya rent isio design.

 

 

 

Comments
Loading...