Kenya's No 1 GhettoRadio

Gavana Joho Amfokea Mvurya Kuhusu Uchaguzi Wa Msambweni

0

Huku ikisalia wiki mbili tu uchaguzi mdogo wa eneo bunge Msambweni ufanyike, Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho na mwenzake wa Kwale Salim Mvurya  wamekabana koo kuhusu uchaguzi huo Mvurya akiunga mkono Feisal Beder ambaye anaungwa mkno na naibu rais William Ruto.

Joho ambaye anapigia debe  yule mgombea wa ODM  Omari Boga amemshambulia Mvurya kuhusu siasa za Pwani akimtaja kama kiongozi ambaye hana nguvu kisiasa kushindana naye.

‘‘Mimi napenda ushindani wewe kama una nguvu njoo ushindane na mimi kule Mombasa mimi naye najiamini niko na watu naja kwako kushindana na wewe si ndio siasa hiyo.. sema niseme  nipe nikupe,’’ aliambia Mvurya.

‘‘Wamepoteza mwelekeo na wengine wameanza propaganda ati sijui Boga ni candidate wa serikali nataka kuwaambia mimi ndiyo nilifanya hapa kampeni za Jubilee lakini rais Uhuru kenyatta hajasema yeye yuko na candidate hapa Msambweni.’’ Mvurya alisema.

Uchaguzi mdogo huo utafanyika tarehe 15 Desemaba.

Comments
Loading...