Kenya's No 1 GhettoRadio

Kenya Imejengwa Loan ingine na IMF

International Monetary Fund yaani IMF wame approve Kenya kukanjwa loan ya Ksh.28 billion.

Hio monyo ni ya utat kwa budget ya miezi 38 support program, na iliitishwa April last year na ati itaokolea kukanja mafuliza zingine.

Hii inamaanisha hio program ya miaka utat ni143 billion.

IMF wanadai wametuskumia hio maziwa after kukemba tunatii program structural reform requirements zao ingewaje tulilalisha kiasi kwa execution.

Wanakemba COVID-19 vaccine spending na completed comprehensive audit ya fiscal year 2020-2021 waki focus sana sana kwa COVID-19 spending wajue kama kuna transparency.

IMF wamekajaza medium term outlook iko bien despite near term risks yenye ina casuiwa na rising commodity prices na drought.

Wasee wamekuwa wakibonda juu ya hizi loans bwaku wakibuya itatusotesha lakini gava imekua ikidai hizi loans ndio zimetulea wakati mambo imekua dimanga.

Comments
Loading...