Kenya's No 1 GhettoRadio

Wafanyibiashara wa Mitumba Waonywa, Serikali ya Kenya Ikifungua Biashara Hiyo

0

By Allan Otieno

Wafanyibiashara wa nguo za  Mitumba katika soko la Gikomba hapa nchini  wametakiwa kufuata kanuni zote za serikali wanaporejea katika biashara hiyo kwani serikali haitakubali  kanuni yoyote kuvunjwa.

Kulingana na Naibu Kaunti Kamishena Kamkunji Moses Lilan kanuni hizo zitazuzia kuenea zaidi kwa ugonjwa hatari wa Korona kwani idadi ya wafanyibiashara Gikomba ni wengi.

‘‘Sisi kama serikali hatuazuia watu kufanya biashara hiyo lakini lazima wafuate sheria za wizara ya Viwanada  na wakifanya hivyo basi sisi hatutakuwa na shIda yoyote nao ..ni amri ya serikali na lazima itekelezwe,’’ alisema bwana Lilian.

Wafanyibishara sasa watahakikisha kila mzigo  itakuwa inaonyesha imetoka nchi gani,ni bidhaa aina gani,kabla ya kuingia sokoni na pia Mitumba yote itakua inapitia shirika la Kebs kwa ukaguzi.

Lilan aidhaa amekataa dhana  kuwa serikali ilikua inakandamiza wauzaji Mitumba ndiposa wakashiriki mgomo.

‘‘Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tutadhibiti kusambaa kwa Korona tufuate sheria na tufanyebisahara wale watakaokiuka  maagizo kutoka KEBS watachukuliwa hatua kali,’’ afisa huyo wa Utawala aliongeza.

Nyae wafanyibiashara wa Mitumba wamekpiunga baadhi ya kanuni hizo wakiesma kuw aitakuwa na gharama kubwa kutimiza.

Kulingana nao biashara ya Mitumba haina mapato ya juu na kwamba ikiwa watalazimishwa na sheraia hizo mpya basi itakuwa vigumu kupata faida.

‘‘Ukaguzi wa Mitumba kupitia shirika la KEBS lazima utozwe ada,kubeba mizigo kutoka banadarini hadi huku sokoni ni gharama  tutafanyeje bisahara serikali tupunguzie  haya masharti,’’ Charles Njau mfanyibiashara Soko la Gikomba  aliambia kituo hiki.

Kumekuwa na maandamano kote nchini wafanyibiashara hao wakitaka serikali kuruhusu biashara hiyo ya Mitumba nchini baada ya kupigwa marufuku mapema Machi mwaka huu.

Comments
Loading...