Kenya's No 1 GhettoRadio

Wakenya Wasimulia Makali Ya  Corona Na  Changamoto Ya  Matibabu Ya  Nyumbani

0

BY CLARET ADHIAMBO

Huku  janga  la Corona likiendelea kuyumbisha maisha ya wengi hapa nchini mawimbi hayo yamekuwa yakienea kwa kasi  lakini  wengine walichuyachukua kwa mzaha mpaka pale walipoona na macho yao jinsi ugojwa huu  unavyotekeleza madhara sio haba.

Hapa Kenya waziri wa afya Muthai Kagwe amekuwa akionya wakenya kila mara kumakini sana na ugonjwa huo na wasirejee maisha yao kawaida kauli ambayo wengi walilimbikiza na wengine  kutafuna.Kutana na Daniel Ochieng ambaye aliambukizwa na Korona  na ghafla ya maisha yake yakabadilika.

Ochieng  alilazimika kufuata kanuni ya serikali  na kukumbatia matibabu ya nyumbani kwake mtaa wa Umoja Tena . Jambo ambalo halikuwa rahisi kukumbati  mkewe Elizabeth Kimuyu akawa  amepatwa na mshangao mkubwa.

Familia yake yote ilipimwa ugonjwa huo kabla yeye  kuruhusiwa kujitenga nyumbani hapo ndipo Daniel alijitenga kwa chumba  kimoja  na hijakuwa rahisi kama wengi wanavyodhani.Bibi yake Elizabeth pia alizongwa na mawazo  kwani  alilazimika kutumia chumba cha wototo ili aweze kujitenga wanao pia ambao hawakuwa wampeata ugonjwa huo.

‘‘Ilibidi nitumie chumba cha watoto kulala kujitenga ,nikachukua vyombo na vifaa vingine kuhakiklisha kuwa sitangamani na bwangu tena lakini imekuwa vigumu kwani unaskumwa kimawazo sana si rahisi lakini nilifanya kadri niwezalo,’’ alieleza Elizabeth.

Kulingana na kanuni za wizara ya afya  yule ambaye yuko katika matibabu  ya nyumbani  lazima awe na  magwanda yanayomkinga dhidi ya kusambaza ugonjwa huo.

Lakini kwa familia ya Ochieng walinunua kila kitu magwanda ya kujikinga yote ikiwemo maski…Ochieng alipozongwa sana na mawazo alitoka nyumbani na kuenda katika kituo cha kujitenga cha St . Georges.

Akaongeza kuwa ‘‘ haikuwa rahisi kwa sababu mimi sikupata mtu  kunieleza vile naweza fanya nilikua nafuatilia tu kutoka kwa taarifa tunazoona kwa televisheni  kuhusu matibabu ya nyumbani.’’

Mbali  na Ochieng  kuna Jay ambaye si jina lake kamili mkaazi wa kinoo ambaye  pia aliambukizwa Korona  na akajitenga nyumbani kwake masaa 24 pekee mtaani Kinoo.

Kulinganana na Jay kesi yake ilikua tofauti kabisa kwani kujitenga na kukabiliana na ugonjwa huo hakukuwa na changamoto kubwa ila mawazo yalimzonga sana.

Yaliyomwongeza mawazo ni taarifaa za kila ziku zinazotolewa  na serikali kuhusu ugonjwa huo kupitia televisheni.

‘‘Habari za covid za kila siku inafanya uwe na hofu sana na naomba ukiwa katika matibabu ya kinyumbani  wacha kutizama  habari hizo kwani zinachangia  mawazo ambayo  yanakuzonga mimi niliathirika sana nikitazama matangazo hayo ya kila siku,’’ Jay alidokeza.

Kinachodhirika wazi ni kwamba wagonjwa wa Corona ambao wako katika mpango wa matibabu ya nyumbani  wanakosa wale ambao wanawapa ushauri nasaha lakini licha  hayo yote, mamia ya  wagonjwa hao wamendelea kupata afueni.Ijuma tarehe 22 Agosti wagonjwa 190 waliweza kupona.

UNYANYAPA

Unyanyapa ni changamoto kubwa ambayo wagonjwa wa  Corona wanapitia.Elizabeth Ochieng  alilazimika kuwaonya wanawe kutozungumzia  swala la  Corona katika familia yao ili kuzuia kutengwa na jamii yake na hata majirani wake.

Ipo haja ya serikali kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu swala unyanyapaa ili wale ambao wako katika mpango wa matibabu ya nyumbani wawe katika nafasi sawa katika jamii .

 

 

 

Comments
Loading...