Kenya's No 1 GhettoRadio

Yut alimdingo hawker amechargiwa

0

Kuna yutman mwenye ali attack hawker akiwa kwa mbogi ya maguangi sita, na wakamnyafura tenje yake ya kappa 40 na wire ya ogoro ya miti 15, amechargiwa kwa kotiko na robbery with violence.

Kelvin Abuga Auma AKA Rio ana accusiwa kumdingo Kelvin Mwangi Warui githare hapo Juja rd on May 19, 2020 wakiwa na kidungi.

Warui alikuwa biz akindonyo face masks ndio akakutwa na hio mbogi na anawatambua fiti.

Walimvaa na wakamtishia na mpini.

Ali identify Rio kwa mambanga, mwenye after kuchargiwa ame wachiliwa na bondiko ya mote soo tatu.

Rio alikwara hizo charges mbele ya judgiko wa Makadara Merissa Opondo

Rio alidai ako na mabro na masiz wanamtegea na kuget hio bond ni hard, lakini judgiko alidai kuna makesi za wasee kulenga kurudi mbwenya wakiwachiliwa na bail ama bond.

Kesi itaendelea September 22, 2020.

 

Comments
Loading...